Baba Mzazi wa Britney Spears Aingia Matatani
Baba mzazi wa Msanii Britney Spears, Jamie Spears ameingia matatani baada ya kutuhumiwa ‘Kumchapa Vibao’ mjukuu wake.
Vyanzo vya habari vinasema Kevin Federline ambaye ni mzazi mwenza wa Britney Spears alitoa taarifa Polisi baada ya kushuhudia tukio hilo lilitotokea tarehe 24, August 2019 katika makazi ya Jamie yaliyopo katika mji wa Ventura.
Mtandao wa TMZ umeripoti kuwa Jamie aliingia kwenye majibizano na mjukuu (Mtoto wa Britney na Kevin) wake ambaye ana umri wa miaka 13, kitendo kilichomfanya apandwe na hasira na kuamua kumchapa kibao. Polisi wa mji huo wamefungua jalada la uchunguzi wa kesi hiyo na endapo atakutwa na hatia, atakabiliana na adhabu kali.
Toa Maoni Yako Hapa