Burna Boy, Tiwa Savage Waapa Kutokanyaga Afrika Kusini
MWANAMUZIKI wa miondoko ya Afrobeat nchini Nigeri, Damini Ogulu maarufu kama Burna Boy ameapa kutokanyaga ardhi ya Afrika Kusini baada ya kutokea ghasia dhidi ya raia wa kigeni.
Kupitia ukurasa wake wa T witter Burna Boy ame tweet akisema hawajawi kukanyaga nchini afrika Kusini tangu mwaka 2017 lakini awezi kwenda tena hadi serikali ya Afrika Kusini itakaposhughulikia suala hilo.
Burna Boy aliendelea kutweet akisema ”Naelewa mateso waliopitia miaka mingi iliopita imewafanya waafrika Kusini kuchanganyikiwa kiasi cha kuwachukulia kama maadui watu waliowasaidia wakati wa utawala wa kibaguzi.”
Aliongezea kuna raia wa Afrika Kusini ni ”watu wazuri na wapenda maendeleo “… lakini kwa hili wamekosea”.
Mwanamuziki Tiwa Savage nae akukaa kimya ameamua kufutilia mbali shoo ya tamasha la DSTV Delicious Festival litakalofanyika jijini Johannesburg September 21 mwaka huu baada ya kuchukizwa na matukio yanaoendelea nchini Afrika Kusini.
Kwenye ukurasa wake wa Twitter Tiwa Savage ame tweet kuwa hawezi kuvumilia vitendo vya kikatili vinavyofanywa dhidi ya Wanigeria wenzake nchini Afrika Kusini.