Sambaza

Dogo Janja : Namtamani Sana Vee Money

MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva, Abdulaziz Chande ‘Dogo Janja’ ameweka wazi mapenzi yake kwa mwanamuziki mwenziye Vannessa Mdee ‘Vee Money’ kuwa ndiyo mwanamuziki anayemtamani sana kufanya naye kolabo.

Akipiga stori na Risasi Vibes, Dogo Janja alisema kila mwanamuziki anaamini akifanya kazi na mwanamuziki fulani anajiachia na lazima mashabiki wafurahie basi kwa upande wake Vee Money ni namba moja.

“Ndoto yangu kubwa ni kufanya kazi na Vee Money, naona wazi tukifanya kazi kwanza tunaendana na pia anaweza kurahisisha kazi kwa sababu nitakuwa najiachia na kufanya kazi kwa uhuru. Naimani ndoto yangu ya kolabo naye itakamilika,” alisema Dogo Janja.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey