Sambaza

Justin Beiber Aeleza Jinsi Ndoa Ilivyombadilisha

Mkali wa Muziki kutoka nchini Canada, anayeishi nchini Marekani Justin Beiber ameamua kuandika ujumbe mzito akielezea jinsi ndoa yake ilivyofanikiwa kumbadilisha na kumfanya awe bora.

Katika post yake aliyoiweka kwenye ukurasa wake wa Instagram, Justin Beiber ameeleza changamoto alizokumbana nazo alipokuwa akiishi na wazazi wake wawili baada ya kutengana akiwa na umri mdogo, vile vile amezungumzia maisha ya ‘Umaarufu’, matumizi ya madawa ya kulevya akiwa na miaka 19 na kutokuwa na heshima na hasira kwa wanawake kipindi akiwa katika mahusiano yake kadhaa ya nyuma.

“Nilitumia miaka kadhaa ili kuweza kurudi kuwa mpya kwa kurekebisha mahusiano yangu kadhaa, kubadilisha tabia ya mahusiano yangu nashukuru Mungu sasa nimezungukwa na watu ambao wananipenda  na zaidi nipo nasafiri katika kipindi bora cha maisha yangu Ndoa,” aliandika.

Justin Bieber na Mchumba wake Hailey Baldwin kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vinaonesha wawili hao tayari ni wanandoa, lakini hakuna uthibitisho uliotolewa kati yao kuhusu suala hilo.

 

 

View this post on Instagram

 

Hope you find time to read this it’s from my heart

A post shared by Justin Bieber (@justinbieber) on

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey