Sambaza

R Kelly Atolewa Kwenye ‘Kifungo cha Pekee’

Msanii nguli wa RnB ambaye amekuwa akiandamwa na kesi ya uzalilishaji wa kingono akishitakiwa kwa makosa 13, R Kelly ametolea kwenye Kifungo cha pekee ‘Solitary Confinement’  na kuchanganywa na wafungwa wengine.

Akiongea na mtandao wa TMZ, wakili wa mwanamuziki huyo Steven Greenberg amesema kifungo alichopewa R Kelly mwanzo ‘Solitary confinement’ ilikuwa ni adhabu ya maafisa wa gereza na haikuamriwa na mahakama apewe adhabu hiyo.

Akaendelea kusema kuwa, kitendo cha R Kelly kutolewa kwenye ‘Solitary confinement’ ni cha hatari kwani kwa mtu maarufu kama R Kelly kuchanganywa na wafungwa wengine kitahatarisha sana usalama wake ila ameahidi kuchukua tahadhari kubwa za kiusalama ili kuhakikisha usalama wa mteja wake unapewa kipaumbele.

Kitendo cha R Kelly kutolewa kwenye kifungo cha pekee na kuchanganywa na wengine kimempa nafasi ya kukutana na mawakili 10 kwa siku ambao watakuwa wakimsaidia katika kesi yake tofauti na mwanzo alipokuwa kwenye solitary confinement, aliruhusiwa kukutana na wakili mmoja tu.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey