Sambaza

Baba Diamond Azungumzia Harmonize Kuondoka WCB

Baba wa Diamond Platnumz msanii wa Bongo anayefanya vizuri, Mzee Abdul Juma amefunguka kuhusu uamuzi wa msanii Harmonize kuondoka kwenye Lebo ya WCB ambayo inamilikiwa na mwanaye Diamond Platnumz.

Akipiga story na moja ya Televisheni ya mtandaoni ya hapa Bongo, Baba Diamond amesema kuwa ;

” Harmonize alianza kuonyesha dalili toka mwanzo za kuondoka WCB baada ya kuanza kufanya show binafsi nchi za nje, kitu kilichomfanya ajione ana jina kubwa kuweza kusimama mwenyewe ” 

Baba Diamond hakuishia hapo, aliongeza kuwa Harmonize ameshakuwa mtu mzima hivyo yuko huru kufanya maamuzi binafsi.

” Naseeb alimpigania sana Harmonize, amepambana kujenga brand yake na kuukuza muziki wake….lakini ameshakuwa na ana uwezo wa kufanya maamuzi..”

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey