Sambaza

Billnas Akanusha Kuhongwa Gari na Nandy

Msanii wa Bongo fleva, William Nicholaus Lyimo aka Billnas amekanusha tetesi za kununuliwa gari na msanii mwenzie Nandy ambazo zimekuwa zikisambaa mitandaoni. 

Billnas ambaye alitembelea studio za +255 Global Radio kutambulisha Wimbo wake ambao ameshirikiana na Nandy unaoitwa ‘BUGANA’ amekanusha tetesi hizo na kusema kuwa hajawahi kununuliwa gari na mwanamke, magari yote aliyowahi kumiliki ambayo idadi yake ni magari saba aliyanunua kwa pesa zake mwenyewe.

Mbali na kuzungumzia kazi yake mpya ambayo inafanya vizuri kwenye vituo mbalimbali vya redio, amefunguka pia kuhusiana na maisha yake ya nyuma;

Hapa nilipofika nimepiga hatua kubwa sana, nilipitia maisha magumu sana kabla ya kuwa staa kitendo kilichokuwa kinafanya mpaka nilale chumba kimoja na dada zangu sababu tu ya ugumu wa maisha.

Kuhusu kushirikiana na wasanii wa Lebo ya WCB, Billnas amesema kuwa hana tatizo na wasanii wa lebo hiyo na alishawahi kufanya collabo na Rayvanny japokuwa haikutoka. Alipoulizwa endapo atahitajika katika lebo hiyo kuziba pengo lililoachwa wazi na Harmonize, Billnas amesama hawezi kuwa mbadala wa msanii fulani kwani anaamini kila amsanii ana ladha yake katika muziki.

Tazama Video ya Interview Nzima Hapa

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey