Tanasha ‘Agoma’ Kutoa Jina la Mtoto
Mtangazaji na msanii kutoka Kenya Tanasha Donna ameweka wazi kuwa hatotoa jina la mtoto wake hadharani kwa kuhofia ‘watu wabaya’ kumdhuru. Tanasha ambaye anatarajia kujifungua siku chache zijazo mtoto wake wa kwanza na Diamond Platnumz amesema hayo alipokuwa akiongea na fans wake kwenye mtandao wa Instagram.
” I am afraid that bad and evil people will harm him, we have already discussed about the name but we can not share it at the moment,” Alipost Tanasha
Diamond Platnumz na Tanasha wanataraji kupata mtoto hivi karibuni na tayari wameshaanza maandalizi ya kununua baadhi ya vitu kwa ajili ya mtoto wao.
Toa Maoni Yako Hapa