Sambaza

Billnas Azungumzia Uwezekano wa ‘KUACHIKA’

Hitmaker wa ‘BUGANA’ Billnas amefunguka kuwa yuko katika wakati mgumu kimahusiano na mpenzi wake kutokana na tetesi zinazoendelea kusambaa kuwa amerudiana na Nandy. 

Akipiga story na moja ya kituo cha radio hapa nchini, Billnas amesema

” Inaniathiri pakubwa kwa sababu mahusiano yangu yapo kwenye changamoto kubwa sana au siku yoyote mkisikia nimeachika msishangae, sisi hatujiachii na hatuko karibu kama ambavyo watu wengine wanaona kwa sababu tangu nimeachia wimbo wa Bugana sijaonana tena na Nandy mpaka leo”, ameeleza Billnas

Mbali na hayo, Billnas amesema hata picha anazopost katika mitandao ya kijamii ni za siku nyingi ambazo walipiga wakati wakishoot video ya BUGANA na kusisitiza kuwa hana ukaribu sana na Nandy kama watu wanavyofikiria.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey