Nicki Minaj Atangaza Kuachana na Muziki
Mwimbaji wa miziki ya miondoko ya Hip Hop, Nicki Minaj amewashangaza mashabiki wake hapo jana baada ya kutangaza kuwa anastaafu biashara ya Muziki ili aweze kuanzisha familia
Minaj (36) ametoa taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter, japokuwa hajawahi kutoa taarifa yoyote kama ni mjamzito au ameshaolewa
Mwezi Juni 2019, alisema kuwa ana mpango wa kuoana na mpenzi wake, Kenneth “Zoo” Petty na mwezi Agosti 2019 alibadilisha jina analotumia Twitter kuwa Mrs. Petty ila hajawahi kuzungumza kama tayari wameshaoana ama la
Minaj aliyeanza safari yake ya Muziki miaka 10 iliyopita ameshinda tuzo sita za ‘American Music’ na pia ameshawahi kuwa mmoja wa watu katika orodha ya Watu 100 inayotolewa na Time mwaka 2016 ya Watu wenye ushawishi duniani