Alikiba Azungumzia Kuhusu Kuachana na Mkewe
Mfalme wa Bongo fleva, Alikiba ameamua kuweka ukweli wazi kuhusiana na tetesi zilizosambaa mitandaoni kwa muda mrefu kuwa ameachana na mke wake, Bi Amina Rikesh waliyefunga ndoa mwaka jana.
Akiongea na kituo kimoja cha redio cha hapa Tanzania, Alikiba amesema “Niko na family kama kawaida, na mtoto anaendelea vizuri namshukuru mungu , kuna watu wanasambaza sana huu uzushi lakini wanatakiwa wafocus kwenye mambo yao na waache kufatilia maisha ya watu” Amesema Alikiba
Toa Maoni Yako Hapa