Kanye West Azidi Kutanua ‘Dhehebu’ Lake
RAPA asiyeishiwa vituko Kanye West, jumapili ya tarehe 8, September ameendelea kutoa huduma ya neno la Mungu kwenye mikusanyiko ambayo amekuwa akiifanya kila jumapili.
Jumapili hii ‘Sunday Service’ yake ilikuwa kwenye mji wa Chicago mji ambao alizaliwa. Katika huduma hiyo iliyofanyika katika uwanja wa Huntington Bank Pavilion ambao ulikusanya wafuasi zaidi ya 30,000. Kanye West alimkaribisha Chance the rapper ambaye aliperform “Ultralight Beam ” wimbo ambao upo kwenye Album ya Kanye ‘The Life of Pablo’.
Kanye amekuwa akipongezwa kwa kuzidi kupata wafuasi wengi wa dhehebu lake hasa baada ya kuanza kufanya ‘Tour’ ya kutangaza neno la Mungu kwenye miji mbalimbali nchini Marekani. Awali Kanye West alikuwa akifanya huduma katika Jiji la Los Angeles pekee na watu waliokuwa wakihudhuria walikuwa ni wachache waliopata mualiko maalumu.