Sambaza

Siri Kubwa ya Ndoa ya Harmonize na Sarah

TUKIO la Msaniii wa Bongo fleva, Harmonize kufunga ndoa na mchumba wake wa siku nyingi  Sarah Michelotti bado linaendelea kuumiza vichwa vya baadhi ya wafuatiliaji wa mambo! Tukio hilo lililofanyika siku ya Jumamosi na kuhudhuriwa na baadhi ya ndugu na marafiki wa karibu wa Harmonize na Sarah limekuwa gumzo hasa baada ya kutokuwepo kwa msanii hata mmoja kutoka Lebo ya WCB na jinsi lilivyofanyika kwa usiri mkubwa.

Ndoa hiyo ya kiislam imefungwa ikiwa ni miezi michache baada ya Harmonize kumvisha pete ya uchumba Sarah alipokwenda kutambulishwa kwa wazazi wake Sarah nchini Italy. Vyanzo vya habari vinasema kuwa Harmonize na Sarah walikuwa wamefunga ndoa ya ‘SIRI’ ya Kiserikali miezi kadhaa iliyopita kutokana na kutofautiana kiimani, kwani Harmonize ni muislam na Sarah ni mkristo, hivyo ndoa hii ya Kiislam imefanyika baada ya Sarah kukubali kubadili dini na kuwa muislam.

Bado haijafahamikia kwa nini wasanii kutoka Lebo ya WCB hawakuhudhuria tukio hilo la ndoa ya Harmonize, na bado haijafahamika kama walipewa mualiko ama La!!

 

 

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey