Sambaza

Jumba la Kifahari la Swizz Beats & Alicia Keys lawa Gumzo

   Alicia Keys na mumewe Swizz Beats wamefanya kufuru ya pesa kwa kununua jumba la kifahari lililopo ufukweni lenye thamani ya dollar za Marekani Milioni 20.8 ambazo ni sawa na Shilingi bilioni 48 za kitanzania.

Jumba hilo liko kwenye ufukwe wa bahari juu ya miamba, eneo linalojulikana kama La Jolla, California eneo ambalo kuna makazi ya matajiri kama Ron Burkle, Christy Walton, na  Jeff Hawn.

Alicia na Swiss Beats wameingia katika list ya mastaa wanaomiliki mijengo ya kifahari duniani baada ya kununua Jumba hilo ambalo limebuniwa na mbunifu mahiri wa majengo duniani Wallace E. Cunningham. Mbali na kununua jumba hilo, ‘Couple’ hiyo ya muda mrefu pia wanamiliki mijengo kadhaa katika maeneo mbalimbali nchini Marekani kama Englewood, New Jersey mji ambao walinunua jumba la Msanii Eddie Murphy kwa dolla za Marekani bilioni 12.1 mwaka 2013 .

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey