Mradi wa Kanye West wa ‘VIJUMBA’ Wavunjwa Rasmi
Mradi wa Kanye West wa nyumba za gharama nafuu aliokuwa amelenga kusaidia jamii yenye kipato cha chini umesitishwa na kuanza kuvunjwa na mamlaka za mji wa Calabasas.
Mradi huo wa ‘Vijumba’ hivyo vilivyokuwa na muundo wa duara ulitangazwa kupigwa marufuku na kuamriwa nyumba hizo zibomolewe kwa sababu ulikiuka sheria za mji huo, pamoja na malalamiko kutoka kwa majirani waliokuwa wakilalamikia shughuli za ujenzi huo kuwa kero katika eneo lao.
Kanye West alibuni mradi huo akiwa na maono ya kuanzisha jamii itakayoishi kwa usawa bila kuwa na matabaka ya kimadaraka na kipato (Egalitarian Society) lengo ambalo limekwama kutokana na kukiuka baadhi ya sheria za makazi za mji huo.
Toa Maoni Yako Hapa