Rapa Fetty Wap Amkana Mtoto Wake Instagram
Baada ya kuweka wazi Rapa Fetty Wap kuwa yeye ni baba mzazi wa wa mtoto Alaiya ambaye alizaa na mwanadada mrembo Alexis Skyy, sasa basi rapa huyo amekana mtoto wake.
Mtandao wa TMZ umeripoti kuwa Rapa Fetty Wap leo kupitia ukurasa wake wa instagram live amefunguka mbele ya mashabiki zake kuwa yeye sio baba mzazi wa Alaiya kama ambavyo wengi walikuwa wakifahamu .
Kupitia insta live Fetty Wap amesema “Nimekuwa nikimpenda Alaiya , Nilikuwepo kipindi anazaliwa na niliweza kwenda hospitali kumuona. Mimi na mama yake tulikuwa wapenzi lakini haina uhusiano wowote na mimi kuwa baba wa mtoto wake. Nikihitaji kumsaidia kwa chochote nitafanya hivyo lakini si kuvuka mipaka. Kama ningekuwa baba wa damu, basi mambo yangekuwa tofauti.”
Toa Maoni Yako Hapa