Billnas Alinipa Dawa Mimba Ikatoka – Nandy
Msanii wa kike anayefanya vizuri kwenye game ya muziki wa Bongo fleva, Nandy ameanika siri ambayo watu wengi walikuwa hawaifahamu kuhusu kushika ujauzito wa msanii mwenzie, Billnas.
Akipiga story na kituo kimoja cha redio nchini, Nandy anasema wakati wakiwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na Billnas aliwahi kushika ujauzito wake lakini kwa bahati mbaya ‘ULITOKA’ baada ya Billnas kumletea dawa ambazo hakujua kama zingesababisha ujauzito ule utoke.
” Nilikuwa excited sana na ujauzito ule na niliumia sana ulipotoka lakini sikuwa na jinsi maana ilishatokea na sitaki kukumbuka tena.. ” Alisema Nandy
Toa Maoni Yako Hapa