Nampenda Sana Vanessa, Mpaka Nimpate – Bright
Msanii wa Bongo fleva Bright ameweka wazi hisia zake kuwa anampenda sana msanii mwenzie Vanessa Mdee ‘Vee Money’ na kuongeza kuwa kwa mwanaume yeyote ambaye ni rijali ni lazima atavutiwa kimapenzi na Vee Money.
Bright ameyasema hayo alipokuwa akipiga story na kituo kimoja cha televisheni hapa nchini na kuongeza kuwa jambo la kumpata Vanessa Mdee linaweza likawa hivi karibuni waombe uzima na kwa mahaba ambayo atampa atamtuliza mwenyewe.
Toa Maoni Yako Hapa