Familia Ya 6ix9ine Inaogopa Kwenda Mahakani Kusikiliza Kesi Ya Ndugu Yao
Mtandao wa TMZ umeripoti kuwa wiki ijayo itaanza kusikilizwa rasmi kesi ya rapa 6ix9ine ila familia yake hataweza kuhudhulia mahakani kwa kuhofia maisha yao
Kupitia mtandao wa TMZ umeripoti kuwa familia ya 6ix9ine inaogopa kwenda mahakani kusikiliza kesi hiyo ya ndugu yao kwasababu wanahofia kupoteza maisha yao, Rapa 6ix9ine amekubali kutoa ushaidi dhidi ya kundi lake la zamani la uhalifu Nine Trey Gangsters Bloods ili aweze kupunguziwa hukumu.
Wiki moja tu iliyopita, meneja wa zamani wa Tekashi na Mwanakundi wa Juu wa Nine Trey Gangsters Bloods, Kifano “Shotti” Jordan alihukumiwa kifungo cha miaka 15 gerezani kutokana na makosa kadhaa ya uhalifu aliyowahi kuyafanya pamoja na 6ix9ine na wanakundi wengine siku za nyuma.
Toa Maoni Yako Hapa