Bodak Yellow Imetengeneza Rekodi Nyingine Kwa Cardi B
BODAK YELLOW ambayo ilikuwa ladha ya kwanza kutokea kwenye albamu yake ya kwanza ya Invasion Of Privacy, imetengeneza rekodi nyingine ya mwanamuziki huyo ambaye tangu kupata nafasi amekuwa akivunja rekodi tofauti kwenye muziki pamoja na mafanikio mengi yasiyokuwa na kikomo.
Wimbo huo uliotolewa mwaka 2017 , Umekuwa Platinum Certified mara tisa, namba inayomfanya Cardi B kuwa MwanaHip-hop wa kike ambaye amepata madaraja mengi ya mauzo ya wimbo mmoja.
Bodak Yellow pia ilimpa CardiB jina la heshima mara baada ya kuingia nafasi ya kwanza kwenye chati ya Billboard Hot 100 mwezi Septemba 2017.
Toa Maoni Yako Hapa