Sambaza

Rostam Na Nay Wa Mitego Kwenye Kijiwe Nongwa

Soka la bongo linakwama wapi, TFF Maana yake nini?, ameuliza Stamina kwenye line ambayo Roma amejibu kwa kusema TFF ni Tanzania Football Failure. Kama ulikuwa haujui Rostam wamerudi kwenye spika zako na brand new hit ‘Kijiwe Nongwa’ ambayo ni kolabo yao ya kwanza na true boy Nay Mitego.

 

kwenye upande wa burudani, sio TFF tu ambao wametupiwa shot kwenye wimbo huu ulioachiwa siku ya Alhamisi, Septemba 19,2019, Watu wengi wamefikishiwa meseji zao na moja kwa moja tunaweza kuelewa Rostam na Nay Wa Mitego wamewaambia nini kina nani. Kijiwe Nongwa ni wimbo wa Hip-Hop uliotengenezwa na Bin Laden pamoja na Mr. Ttouch, wimbo huu umebeba stori nyingi ikiwemo ya mastaa wawili waliowahi kutrend na ndoa yao ambapo tofauti ya umri wao iligeuka gumzo, Mwanamke alikuwa ni mama wa mtoto mmoja ambaye baba yake alifariki, na mwanaume aliyekuja kumuoa mwanamke huyo alikuwa ni mdogo kiumri.
chukua point hiyo fananisha na mistari hii
”na kuna demu aliachiwa mtoto
akaolewa na mtoto,
akaachana na mtoto
akabaki anamlea mtoto” (Roma amejibu kauli hii huku anacheka).
Ukiunganisha matukio unakumbuka kuhusu ndoa hiyo ambayo imevunjika na kila mmoja anaendelea na maisha yake.Unataka kujua ni Kina nani hao?, bila shaka hawa ni Irene Uwoya na Dogo Janja ambao inasemekana sasa hivi haziivi tena.

 

Vipi dada yetu wa igunga, simuoni udangani?
Mbona ashapata mchumba sio vibenten wa zamani,
Yule fundi gereji chawa si kamteka bibie,
na wamefungua mgahawa yaani wote mama ntilie,

Tukirudi kwenye line hizo hapo juu tunakutana na Boss wa ShishiFood Shilole na mume wake Uchebe ambaye ameziba nafasi ya Vibenten kwa mrembo huyo mwenye asili ya Igunga Tabora, nani kibenten wa shilole?, aliwahi kuwa Nuh Mziwanda au kuna mtu mwingine?.
Shot nyingine zimeelekezwa kwa Diamond Platnumz na wapenzi wake, Wema Sepetu ni Miss Tanzania aliyeokota almasi mchangani wakati Zari ni mganda aliiyekuja kuinunua dukani kwa nia ya dhati, lakini hawa maharamia waliojitekeza hapa kati huyu mwamba akawanyanyasa kijinsia ni kina nani?.

 

Tukiachana na Diamond na watu wake Roma na Stamina wamegusia ndoa zao kwa kuulizana maswali na kupeana majibu yasiyoeleweka. Kwenye dakika ya 02:01 ya ‘Kijiwe Nongwa’, Stamina anauliza ‘sa sikiza man, vipi shem mama Ivan?, Roma anajibu, ‘aah tupo tupo tu ila hatupo kama zamani, na kuuliza Nawe vipi kwani mbona wife simuoni nyumbani? Stamina anajibu kwa kusema, ‘hey chil man, sina majibu, deal done’. Tunachofahamu KUHUSU Roma na mke wake hatujasikia mgogoro licha ya mwenyewe kusema hawapo kama zamani, hatujui wanapitia nini, Tukirudi kwa Stamina tunakosa majibu tunaposikia “sina majibu , deal done”. Stamina anatuambia vitu viwili hapa moja ni kwamba yeye na mke wake wanapendana kiasi hawezi kujibu chochote au deal done kwa maana ya kwamba wamemalizana na ndoa imeishia hapo?,
Wengine ambao shot zao zimepigwa kwao ni wale waliowahi kumsema vibaya marehemu, Rostam wametukumbusha kuhusu Ruge na wanamuziki waliokuwa wakitofautiana. Roma anaanza kwa kuuliza Marehemu walimsema mnyonyaji kwani muziki una maziwa?, Stamina anapokea mstari huo kwa kusema ‘sasa mungu kamuhitaji na bado hawajafanikiwa, Stamina anaendelea kuuliza ‘hivi we unadhani ndani ya mjengo nani ataliziba pengo?. Sad stori ni kwamba ndani ya mjengo hakuna atakayeziba pengo hilo kutokana na kauli ya Roma inayosema ‘acha maisha yaendelee jasiri ameumaliza mwendo’.

 

C.E.O wa FreeNation Nay wa Mitego kama kawaida yake ametembea na korasi ya kibabe, unaweza kuimagine mzuka wa Nay kwenye kolabo na Rostam ni mwendo wa kuongea ukweli tupu.
Kama kuna kitu Rostam hawatakiwi kukosea ni kuacha kutembea Nay Wa Mitego kwenye perfomance za ‘Kijiwe Nongwa’, kolabo hii inatakiwa kutendewa haki na watatu wote hawa wote kwa pamoja kwani kama ni Chemistry, hii ipo lit.

 

Video Ya Kijiwe Nongwa imeachiwa Septemba 20, Unaweza kuicheki hapa:

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey