Sambaza

Ebitoke: Mabadiliko, Kuondoka Timamu Na Tofauti Ya Majina Yake

Muziki ni sehemu ya maisha ya kila siku, kwa kulitambua hilo +255 Global Radio inahakikisha  kiu yako ya muziki mzuri inakatika kutokana na ukali wa madj wetu akiwemo Dj Super ambaye Ijumaa ya Septemba 20 alionyesha maajabu yake kwa mixing kali kwenye kipindi cha Mid Morning Fresh kinachokwenda hewani saa nne asubuhi mpaka saa sita mchana monday to friday. Watangazaji wa kipindi hicho Dar Boi, Babu Ally na Diane Mkeu walipiga stori na muigizaji Ebitoke ambaye alifungukia mambo mengi ikiwemo maisha yake binafsi, uhalisia, marafiki, mahusiano yake na Yusuph mlela na stori nyingine nyingi.

Ebitoke kwenye kipindi cha Mid Morning Fresh Ya +255 Global Radio.

Ebitoke ambaye jina lake halisi ni Annastazia Exavery, alifungukia utofauti kuhusu uhusika wa majina yake kwa kuweka wazi tofauti kati ya jina lake halisi ambalo ni  Anastazia na jina maarufu la Ebitoke. Hii ilikuja baada ya mtangazaji Diane kuanzisha maada ya mabadiliko kwenye post za Ebitoke ambaye wakati huu anatupia post zinazomuonyesha kwenye maisha ya kawaida tofauti na mwanzo alivyokuwa akijipost na muonekano wake wa kuchekesha.

Diane alianza kwa kumpongeza Ebitoke ambaye sasa hivi anaonekana ‘kutransfom‘ moja kwa moja kutokana na mabadiliko hayo kwa kile alichokiita ni ukuaji wa Ebitoke ambaye post zake za sasa zinamuonyesha Ebitoke mrembo ambaye anastahili kuitwa Annastazia Exavery. Ebitoke aliweka wazi utofauti wa majina yake kwa kusema Annastazia Exavery ni msichana anayeigiza filamu za siriazi na Ebitoke anaigiza filamu za kuchekesha kwahiyo linapokuja suala la kuigiza anatumia majina hayo kutokana na uhusika wa filamu anayoicheza.

Ebitoke amesema aliingia mtandaoni akakutana na tangazo la kutafuta vipaji vya waigizaji kitu ambacho hakukichukulia poa na kuamua kuibuka kwenye usaili siku ilipofika, Ebitoke anasema sanaa yake ilianzia Timamu ambapo alichaguliwa kuigiza Komedi kitu ambacho hakuwahi kufikiria kukifanya.

“Mungu si Athumani nilipokuwa nafanya kazi za ndani  siku moja nikawa napitia kwenye mitandao nikaona tangazo wanahitaji watu kwa ajili ya kufanya usaili amabapo ni Timamu, nilienda kwenye usaili wakanipa nafasi nikaonyesha uwezo wangu bahati nzuri wakaniweka upande wa komedi japokuwa me sijawahigi kuwaza kama nitakuja kufanya komedi”. alisema Ebitoke huku akicheka kwa furaha.

Walitoa jaribio ambalo ni la komedi ,perfomance yangu ilikuwa tofauti na wengine, nilitumia lafudhi yangu ya kiebitoke, nilichekesha watu wengi sana, niliwekeza nguvu nyingi kwa kile ambacho nilikuwa nataka mpaka nikawashinda wengine hadi kumshawishi mtu aliyekuwa akinisimamia kuuuona uhitaji wangu na kunipa nafasi nyingi za upendeleo“. aliongezea Ebitoke.

Baada ya kwenda Timamu kulitokea migogoro baadaye ambayo ilisemekana Ebitoke na Boss wa Timu haziivi, Ebitoke amekanusha kuwepo na ugomvi kati yake na Timo lakini alithibitisha ugomi kati yake na mke wa meneja wake aliyekuwa akimtuhumu kutembea na mume wake.

Ebitoke alisema hakuwa anatoka kimapenzi na Meneja wake bali yeye  anapendwa sana na wanaume kuliko wanawake, ilitokea  amekuwa karibu sana na Timo kitu ambacho kilitemsababishia tuhuma hizo ambazo baadaye zilimchosha na kuamua kuondoka chini ya usimamizi wa Timamu ili awaache wanandoa hao kwa amani.

Angalia Interview Yake Yote Hapa Global TV Online.

 

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey