Sambaza

Gigy Money Awataka Watoto Kutoiga Maisha Yake

Tumekuwa na namba kubwa ya vijana wadogo ambao tayari wamekata tamaa ya kuendelea na maisha kwasababu imekuwa muda mrefu wanahangaikia ndoto zao na bado hawatimizi. Matumizi ya vilevi kama pombe, madawa na Bangi  imekuwa suluhisho la muda mfupi kwenye nyakati ambazo hujikuta wamekosa kabisa matumaini na wengine wamekuwa wakijitoa uhai.

Kujifananisha na watu  waliofanikiwa ni moja kati ya changamoto inayowakwamisha vijana wengi kuwekeza muda wao kwa ajili ya kujiendeleza badala yake wanapoteza muda kuanza kuwafikiria waliowazidi.

Kwenye intavyuu na Bongo255, Gigy Money amewaonya watoto wadogo wanaoupenda muziki wake kwa kuwaambia wasijifananishe na yeye kwani anaishi maisha ya uongo.

“Maisha ya mitandao ni magumu sana, watu wanaongea ovyo Nashukuru Mungu nilijua hicho kitu mapema hivyo sijipi stress kwakweli lakini kama kuna watoto wapo shule wananipenda mimi, ningewashauri waendelee kusapoti muziki wangu waachane na maisha yangu kwani  siyo real”. amesema Gigy Money

Gigy ameongeza kuwa kuna wasichana wanamuona Gigy wa Instagram wanajua anaishi maisha hayo wanayoyaona mtandaoni na wenyewe wameamua kuishi hivyo mwisho wake wameishia kwenye ulevi na umalaya ili kujifananisha na Gigy ambaye muda huu anautumia sana kutafuta hela kuliko kitu chochote.

Gigy Money sasa hivi anatamba na wimbo wake ‘Shoga’ ambao uliachiwa Julai 23, 2019. Unaweza kuicheki video yake hapa chini:

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey