Sambaza

Kim Kardashian Kuonekana Kwenye Video Ya Tupac

Kwa zaidi ya miaka 12 sasa, maisha ya Kim Kardashian yamekuwa kama kitabu cha wazi kwa maana watu wengi wanafahamu vitu vingi ambavyo mrembo huyo amekuwa akivifanya, lakini hivi juzi ametoboa siri ambayo wengi tulikuwa hatuijui, Kim Kardashian ambaye ni mke wa Rappa Kanye West amethibitisha kuwepo kwenye moja ya video za Tupac Shakur alipokuwa msichana mdogo.
Kim alishare stori hiyo kwenye intavyuu alipoulizwa kama kuna kitu kinachomuhusu ambacho watu wanatakiwa kukijua.

….. kuna vitu vingi sana. Wakati nina miaka 14, nilicheza kwenye video ya Tupac. Ilikuwa kama 1994 hivi”. alisema Kim. “Hakuna mtu angejua hili kwani nilikuwa mdogo na nilidanganya umri wangu nikisingizia nina miaka 18” alisema Kim

Kim amesema hakupata nafasi ya kuiona video hiyo wala hajui jina la wimbo na kibaya zaidi hakuipata nafasi ya kumuona Tupac ambaye hakuwepo wakati wa kurekodiwa video hiyo.

“Sikuona video, ninachokumbuka tulikuwa wasichana kadhaa tunatembea kama wanamitindo ndani ya bikini kwenye pool, nilikuwa mimi, Kourtney, Kim Stuart na wasichana wengine”. aliongeza Kim

Video ya Tupac inayosemekana kumuonyesha mwanamitindo Kim Kardashian ni hii ya wimbo “All About You” ambayo Kim Kardashian amekanusha kuwa siyo yeye ambaye watu wanamfananisha .

 

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey