Sambaza

Lil Pump Amejitangaza Mfalme Wa Miami Na Mkataba Wa Bilioni 45

Gazzy Garcia, anayejulikana kama Lil Pump, ni rapper wa Mrekani na mwandishi wa nyimbo. Anajulikana kwa tabia zake zisizo za busara  ambapo mara nyingi huonyesha kutumia dawa za kulevya, hasa bangi. Lil Pump ametangaza kujitoa kwenye Label ya Warner Records iliyokuwa ikisimamia kazi zake.

Lil Pump aliyasema hayo jumamosi iliyopita wakati akijitangaza kama mfalme wa miami ambako ni asili yake, Rappa huyo mwenye umri wa miaka kumi na tisa alisema ” Ni**as tafadhali muache kucheza na mimi , Nilipata watu karibu 150 wote wanataka kunipiga risasi  huko Miami,  Acha kucheza nami kwani mimi ndiye mfalme wa Miami”

Kuhusu  kujitoa Warner Records, Lil Pump amesema sasa hivi anafanya kazi kama msanii binafsi wala hahitaji wakala kwa ajili ya kumuunganisha na label nyingine ambapo anadai hataweza kusaini mkataba wowote kama label zinazomuhitaji zitashindwa kumpa dola milioni 20 ambazo ni zaidi ya bilioni 45  za Tanzania.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey