Sambaza

Maamuzi Mapya Ya Vanessa Mdee Kuhusu Jux

Mambo huenda yakawa mabaya zaidi kuliko tunavyofikiria kwa upande wa mastaa wa Bongofleva Juma Jux na Vanessa Mdee ambao wanapitia kipindi kinachoweza kuwa kigumu baada ya kutangaza kukatisha mahusiano yao kitu ambacho kimefanya tuendelee kuwategea macho na masikio kujua nini kitatokea tena kati yao. Tumegundua kama Vanessa Mdee ameamua “Kui-Unfollow ” instagram account ya Jux yenye followers zaidi ya milioni 4.

 

Baada ya kuyagundua maamuzi hayo ya Vanessa, hatukujiridhisha kama Jux naye anaweza kuwa amefanya kitu kama hicho lakini baada ya kufuatilia akaunti yake tulikuta jina la Vanessa kwenye orodha ya watu zaidi ya mia nne ambao Jux anawafuatilia.

Takribani miezi miwili inasogea tangu Vanessa alipothibitisha kuachana na Jux ambaye walikuwa kwenye mapenzi kwa zaidi ya miaka mitano huku mapenzi yao yakiwa moja kati ya Couple zilizokuwa zikitolewa macho kipindi hicho. Baada ya kuachana na Vanessa, Jux alitumia nafasi hiyo kumuonyesha mrembo wake mwenye asili ya Asia huku Vanessa akipewa skendo ya kutoka kimapenzi na Majizzo tetesi ambazo alizikanusha kupitia Instalive.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey