Sambaza

MCM: Ommy Dimpoz Kuhusu Maisha Na Muziki

Omary Faraji Nyembo amezaliwa 12 Septemba, 1987,  ni muimbaji wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Tanzania ambaye anajulikana kwa jina la kisanii kama Ommy Dimpoz. Ommy alianza kuvuma kwa wimbo wake wa Nai Nai aliomshirikisha Ali Kiba, . Ommy ni moja kati ya wasanii ambao wanajali sana faragha za maisha yao.

Mwaka 2016 kulikuwa na gumzo kubwa baada ya Nay wa Mitego kumuimba vibaya Ommy kwenye wimbo wake na kumshutumu kama shoga. Baadaye Ommy akajibu kwa kuonesha picha ya demu wake na ikaja kugundulika kuwa Nay wa Mitego ana kibamia.  Ommy ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Pozi kwa Pozi Entertainment ambayo meneja wake (Mubenga) aliachia ngazi mwaka wa 2016.  Tangu wimbo wa Cheche (2017), amekuwa chini ya lebo ya Rockstar4000 ambapo Alikiba ni mmoja ya wakurugenzi wake.

Mwaka wa 2018, ulikuwa mgumu sana kwa Ommy Dimpoz. Afya yake ilitetereka sana baada ya kufanyiwa vipimo Tanzania na kuonekana ana kansa. Lakini baada ya kwenda Kenya kwa moja ya marafiki zake wanaofanya kazi pamoja katika muziki ili kufanyiwa uchunguzi zaidi, napo daktari wa huko alipendekeza apelekwe Afrika Kusini kwa uchunguzi zaidi.

Akiwa Afrika Kusini aligundulika kama ana tatizo katika njia kuu ya kupitishia chakula. Daktari wa Afrika Kusini walitengeneza njia mpya ya kupitishia chakula badala ya ile njia ya asili. Ili kufanikisha hili, ilibidi utumbo uvutwe juu. Hivyo kina cha tumbo kimepungua kutoka hali ya umbo halisi. Hata uwezo wa kula umepungua, akila anashiba mapema sana tofauti na watu ambao hawajafanyiwa upasuaji huu.

Kabla ya upasuaji, Ommy alilamikia sana kukosa pumzi, sauti kuwa chini na kadhalika. Hali halisi alifanyiwa upasuaji wa koromeo. Hali ambayo ilisababishwa na sumu iliyowekwa kwenye chakula. Ommy hajui ni wapi alifanyiwa hivyo. Baada ya kufanyiwa matibabu na kurudi kwenye hali yake ya awaida Kwa kushirikiana na Christian Bella, Ommy Dimpoz aliachia wimbo “Ni Wewe’ kwa kumshukuru Mungu na mashabiki kwa dua zao.

Ommy Dimpoz sasa hivi anatamba na wimbo wake ”Show Me” ambao ni wimbo wake wa sita tangu atoke hospitalini. Unaweza kuicheki video yake hapa ambayo inatrend nafasi ya 46 kwa wiki ya pili sasa.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey