Sambaza

Snoop Dogg Amemuingiza R. Kelly Kwenye Ishu Ya Tekashi

Mastaa na mashabiki wa muziki wa Marekani wamekuwa wakijadili kuhusu ishu ya 69 Tekashi ambaye wiki iliyopita aliwataja watu wanaodaiwa kuwa memba wenzake wa kundi la Nine Trey Blood lililokuwa likijihusisha na masuala ya uhalifu siku za nyuma kabla ya Rappa huyo na wenzake hawajawa maarufu.

Tekashi ambaye alikuwa kwenye kipindi cha majaribio, alitakiwa kuwataja watu aliokuwa akishirikiana nao wakiwemo Casanova, Jim Jones, Trippie Red na mshindi wa tuzo ya Grammy Cardi B ambao wote walikanusha taarifa hizo baada ya kutajwa kama memba wa kundi la Nine Trey Blood

Baada ya Tekashi kuwataja wanamuziki wenzake kama wanachama wa kundi la kihalifu aliokuwa akishirikiana nao,  ndipo hapo zikazuka taarifa za unafiki wa Tekashi kitu kilichopelekea mkongwe wa muziki wa Hip Hop Snoop Dogg kuingiza utani wake kwa kupost ‘meme’  inayomuhusisha Tekashi huku R. Kelly akihusishwa kwenye utani huo kwa kauli ya  “R. Kelly peed on me too.”

Kauli hiyo inafananishwa na kesi inayomkabili R.Kelly  ya kuwatumikisha kingono wasichana wadogo, kwa kauli hiyo Snoop alimaanisha Tekashi ni mnafiki kiasi kwamba angejitaja miongoni mwa wale wasichana wa R. Kelly

 

View this post on Instagram

 

????????

A post shared by snoopdogg (@snoopdogg) on

Rappa 69 Tekashi alikamatwa na polisi mwezi Julai mwaka huu akihusishwa kwenye matukio ya uhalifu yakiwemo matumizi ya silaha za moto na ameendelea kuwa stori kubwa kufuatia kesi yake kuchukua mlolongo mrefu. Inasemekana 69 Tekashi yupo uraiani kwa kipindi cha majaribio huku baadhi ya watu aliowataja wakimtaka ajitokeze mwenyewe kabla hawajamfanyia kitu mbaya.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey