Gari Feki La Mgahawa, Harmonize Ametudanganya ?
“Kidogo na Kingi Mungu Ndie hutoa …!!! Nayeye Ndie Kamuumba Masikini na Tajiri…!!!! Hata hapa Nilipo ni kwaneema Zake Sitokula na Kusaza ikiwa kunawengine Kula Yao Ni Yashida #NitagawanaNao …!!! #KONDEBOYMGAHAWA coming on your street in few days ONE LOVE ?? Woow….!!! ?? @kondegang”, hiyo ni kauli ambayo Harmonize aliandika kwenye picha ya jana aliyopost gari lenye nembo ya KondeBoy iliyoongezwa neno mgahawa.
Sasa kabla hata ya mgahawa huo kuanza kuonekana mitaani kama Harmonize alivyoahidi, stori iliyoibuka muda huu n i uongo ambao Harmonize ametumia kuwadanganya mashabiki wake kwa kuposti gari ya kampuni moja ya usafirishaji kama unavyoweza kuona hapa.
Hii inaonekana kuwa picha iliyotengenezwa kwa kubadilishwa rangi ya gari na maandishi, ukiangalia aina ya gari ni moja pia location ni moja. Kuna ishara kama Harmonize amedanganya juu ya ishu ya mgahawa, au kuna kitu cha ziada tunatakiwa kujua?
Endelea kutufuatilia, muda wowote tutakuja na taarifa zaidi zikitufikia.