Sambaza

Kanye West Anakuja Na Albamu Ya Gospel Baada Ya Kuokoka

Siku chache baada ya mwanamitindo wa Marekani Kim Kardashian kuthibitisha kuwa yeye na mumewe Kanye West wameokoka, Kanye  amethibitisha tarehe rasmi ya kuachiwa albamu yake ya Gospo iliyopewa jina la ‘Jesus Is King‘.  Albamu hiyo yenye nyimbo 12 imepangwa kuachiwa September 27,2019.

Kanye ambaye anatambulika kama Yeez, alitangaza taarifa hizo kupitia website yake ambapo alisema albamu hiyo ilipaswa kuachiwa mwaka jana kwa jina la Yandhi. Kim Kardashian pia alipost picha inayoonyesha karatasi yenye tracklist ya albamu hiyo.

Kanye anaendesha huduma za maombi kila jumapili  nyumbani kwake huku mashabiki wakijiuliza ni lini Kanye ameanza kuwa karibu na ukristo, Kanye West ambaye ni Baba wa watoto wannne  amekuwa akiongoza huduma za kuabudu na kuwakaribisha wanamuziki wenzake wanaokuwa wakiubariki ugeni wao kwa fleva za Gospel.

Kim Kardashian alimwambia mtangazaji aliyetaka kujua kuhusu huduma ya maombi ambayo Rappa huyo amekuwa akiifanya nyumbani kwake kuwa Kanye alianza harakati za kujikomboa mwenyewe kwanza, baade akaanza kushirikiana na marafiki pamoja na familia, “Safari yake ya mabadiiko ilikuwa ya kushangaza sana, hatimaye tumeokoka sasa na Kristo ndiyo kitu tunachokiishi” alisema Kim.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey