Sambaza

Kanye West Ameshinda Kesi Inayohusisha Kustaafu Muziki

Takribani miezi minane imepita tangu uzuke ugomvi wa kisheria kati ya Kanye West na EMI,kampuni ambayo ni wasambazaji wa muziki wake. Taarifa zilizotufikia, Kanye na EMI wamefikia makubaliano na huenda ugomvi wao ukafika mwisho. Ripoti iliyotolewa inadai pande zote mbili zimekubaliana kuvunja mkataba wao ndani ya siku 90.

Kanye West attends the Ralph Lauren 50th Anniversary Event held at Bethesda Terrace in Central Park during New York Fashion Week on Sept. 7, 2018. 

Mwezi Januari Kanye West alifunga mashitaka akitaka kujiengua kwenye kampuni hiyo ambayo amekuwa akifanya nayo kazi tangu mwaka 2004 alipoiachia albamu ya kwanza  ‘College Dropout”.  Kanye anadai mkataba wake na EMI unamzuia kustaafu muziki kitu ambacho hataki  kukubaliana nacho.  Bado haijatambulika kama Kanye West anajipanga kustaafu masuala ya muziki muda huu, lakini tunachokifahamu ni ujio wa Albamu yake ya nyimbo za dini “Jesus Is King” itakayoachiwa Septemba 27 mwaka huu.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey