Billnass Pekee Ndiye Niliachana Nae vizuri – Petitman Wakuache
Petitman Wakuache ni miongoni mwa majina yanayotajwa kwa muda mrefu sana kwenye anga ya Bongofleva kutokana na mchango wake wa kuunga mkono harakati za baadhi ya wasanii. Umaarufu wake ulikua alipoanza kushrikiana na Wema Sepetu kama mmoja ya watu wake wa karibu ambapo alipata nafasi ya kusimamia wasanii waliokuwa chini ya Endless Fame ambayo inamilikiwa na Wema Sepetu.
Petitman amesema hakuna kazi ngumu kama kuwasimamia wasanii ambao hawajafanikiwa kwani mafanikio yanapoanza kusogea huwa wanasumbua sana. Petitman ameyasema hayo alipokuwa akijibu kuhusu kumpendelea Country Boy anayeonekana kuwa mwanamuziki mwenye mfanikio kuliko wanamuziki wote aliowahi kufanya nao kazi.
“Wasanii wana mambo mengi sana, mimi nimefanya kazi na wengi nilikuwa na Nuh Mziwanda na Mirror, Billnass pekee ndiye mtu niliachana nae vizuri wengine wote hawa walinionyesha vitu ambavyo sikutegemea wangenionyesha baada ya mafanikio” alisema Petitman.
“Sio kama nampendelea Country, hapana kuna levo nilitaka afike ndio maana sikutaka kuongeza msanii mwingine, ukimuangalia Country Boy sasa hivi hafanani na Country wa miaka mitatu, anafanya vizuri sana kiasi cha kunishawishi kuongeza wasanii kama Young Lunya na msanii mwingine wa Kike ambaye ni Jolie”. aliongeza Petit