Sambaza

Petitman Hawezi Kumuhudumia Mtoto Wake Na Esma?

 

Septemba 23,2019 kwenye kipindi cha Katambuga kinachorushwa +255GlobalRadio, Petitman aliongea mambo  mengi ikiwemo ndoa yake mpya pamoja  na mahusiano na mama mtoto wake Esma ambaye amemtaja kutokuwa na maelewano naye kiasi cha kumnyima hata uhuru wa kumuona mtoto wao Baby Taraj.

“Natoa kila kitu kuhusu mtoto lakini hivyo sio vitu vya kusema, mimi ninachoumia kama Baba nahitaji nafasi yangu kumuona mtoto lakini sipati nafasi hiyo mpaka mtoto akiwa kwa bibi yake Mama Dangote”.  Batikayo ameyasema hayo baada ya kuulizwa kuhusu uvumi kwamba hana maisha ya kumlea mtoto wake kwa maana  hayuko vizuri kiuchumi hadi ameamua kuoa mwanamke mtu mzima kwasababu mwanamke huyo ana uwezo wa pesa nyingi.

Akijibu swali  hilo Petitman amekanusha kutofuata hela kwa mwanamke huyo kwani yeye hajafulia kiasi hicho kwani ofisi yake inamuingiza hela nyingi tu. Pia amemshukuru Mama Dangote kwa mapenzi ambayo amekuwa anamuonyesha tangu siku ya kwanza hadi ndoa yake na Esma ilipovunjika Mama huyo ameendelea kuwa upande wake kwa mapenzi ya ajabu sana.

 

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey