Sambaza

Vanessa Mdee Alivyoichangamsha Bongofleva

Vanessa Mdee A.K.A Cash Madame au VeeMoney, ni msanii wa kurekedi mwenye asili ya Arusha Tanzania. Vanessa ni muimbaji, mwandishi wa nyimbo na mshiriki wa masuala mbalimbali ya kijamii yanayohusu vijana na maendeleo, Umaarufu wake ulianza kuwa mkubwa zaidi alipokuwa akifanya kazi ya utangazji kwenye kituo cha MTV kama mtanzania wa kwanza kufanya kazi na kituo hicho.


Baada ya kufanya kazi za radio na TV tofauti huku akipata deals za ku-host TV shows kama Dume Challenge,Epic Bongo Star Search na Kili Music Awards, Vanessa aliugeukia muziki wa Bongofleva kwa kuanza kusikika kwenye nyimbo kama Money ya AY na Me And You ya Ommy Dimpoz wimbo ambao ulichaguliwa kuwa wimbo bora kwenye tuzo za KTMA mwaka 2013.
Mapokezi ya Vanessa Mdee kwenye game ya Bongofleva yalikuwa ya heshima baada ya ‘Closer’ kama wimbo wake wa kwanza kupata zaidi ya downloads 30,000 kwenye wiki yake ya kwanza, rekodi ambayo inasemekana haikuwahi kuvunjwa na msanii yeyote kabla.

 

‘Closer iliendelea kubaki kwenye chati za radio na TV mbalimbali Bongo kwa wiki 13 mfululizo huku ikimpa Vanessa Mdee nomination 4 za KTMA. Closer ilishinda kipengele cha wimbo bora wa Pop mwaka 2013.
Kutokea hapo, amekuwa akifanya kazi kwa bidii mpaka alipothubutu kukifanya kile ambacho wengi wa wanamuziki wapya na wakongwe wanakiogopa, Vanessa aliweza Kuiachia Albamu yake ya kwanza Money Mondays yenye nyimbo 18 ambayo iliingia sokoni Januri 16,2018, Kwa mujibu wa BoomPlay Tanzania, Money Mondays ndiyo Albamu yenye mafanikio makubwa na imevunja rekodi nyingi za muziki wa Afrika Mashariki katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.Uzinduzi wa Albamu hiyo ulifuatiwa na uthibitisho wa Vanessa Mdee kusaini na Universal Music kama wasambazaji wa kazi zake ambao wataanza kuiachia #ExpensiveEP mwaka huu.


Tukiongea kuhusu Money Mondays, Vanessa alitengeneza kitu adimu kuwahi kutokea kwenye historia ya Soko la Albamu za Bongofleva. Uzuri wa Money Mondays upo kwenye uandishi wa mashairi, mpangilio wa kolabo pamoja na uandaaji wa maprodyuza tofauti.
Wimbo kama Wet na Gnako unaweza kuwa Fullstop ya maswali mengi kuhusu maana halisi ya Hitsong, Kila mmoja kwa nafasi yake anaweza kuthibitisha vile ambavyo wimbo huu uliteka hisia za watu wengi kwa miezi kadhaa licha ya kuwepo ushindani wa nyimbo nyingi nzuri kipindi kile cha mwezi April 2018 ilipoachiwa.

WET inaendelea kuwa miongoni mwa nyimbo bora kuwahi kutokea kwenye historia ya muziki wa Bongofleva, muungano wa Vanessa na Gnako kwenye mdundo wa Dancehall uliotengenezwa na Nahreel ni kitu kikubwa sana kwa level ya muziki wa Tanzania.
‘Scratch My Back’ na Goodlife ni miongoni mwa nyimbo unaweza kusikiliza siku nzima ili mradi tu kila sehemu muziki unaruhusiwa, Vanessa Mdee ameimba kwenye wimbo huo huku akipata support ya kundi la Goodlife la Uganda lililokuwa likundwa na Weasal na marehemu Radio.

‘Kwangu Njo’ na Mohombi ni ngoma nyingine mtu hatakiwi kuimiss kutokea kwenye Monay Mondays, Vanessa na Mohombi wamefanya kazi nzuri humu, Kwa mujibu wa mashairi, Vanessa na Mohombi wanaielezea hali ya mwanamke na mwanaume ambao wako hoi Kwenye mapenzi yao, imefika ile hatua kila mtu anajikabidhi kwa mwenzake.,
‘Pumzi ya mwisho’ na Joh Makini pamoja na Cassper Nyovest ni mwiba mwingine ule unaweza kuwachoma ‘fake female rappers’ wanaoitaka Level ya The Original Cash Madame Vanessa Mdee ambaye ameungana na marapa hao wakubwa Afrika wakibembea kwenye mdundo wa Trap ulitayarishwa na Zombie S2Kizzy.

 

Vanessa ni mwanamke pekee kwenye Bongofleva mwenye kolabo nyingi za ndani na nje ya Bongo, Kutokea Tanzania Vanessa amepata bahati ya kukutana, kupiga stori na kurekodi na baadhi ya wanamuziki wenye majina makubwa Africa kama Mr P, Ice Prince, DJ Maphorisa, Cassper Nyovest, KO, Reekado Banks, Legendury Beatz, Diamond Platnumz na wengine wengi.
Baada ya kushirikishwa kwenye Albamu ‘SPOTLIGHT’ ya Reekado Banks kwenye ngoma MOVE mwaka 2017, Vanessa aliungana na Mnaijeria huyo kutengeneza Bambino, Wimbo ambao upo kwenye Money Mondays, Bambino ni miongoni mwa nyimbo za Money Mondays zilizobahatika kufanyiwa video.

 

Kwa mujibu wa Rapper CPwaa, Vanessa ni toleo la kike la Diamond Platnumz, Mafanikio yake kwenye muziki yamemuwezeshaVanessa kuanzisha record Label aliyoipa jina lake la ukoo ‘Mdee Music’ ambayo mpaka sasa ina wanamuziki watatu akiwemo Vanessa mwenyewe, Brian Simba, na Mimi Mars ambaye anaeitendea haki nafasi yake ya usichana kwenye muziki.
Vanessa ni mwanamuziki wa Bongofleva anayeandikwa mara nyingi kwenye blogs/website za ndani na nje ya Tanzania kitu kinachomfanya kuwa kwenye orodha ya mastaa wa Afrika wanaotrend sana.

 

Mwezi Machi mwaka 2018, Vanessa Mdee alikua miongoni mwa wanamuziki walioikamilisha Albamu ya kwanza ya Diamond Platnumz A Boy From Tandale, Kwenye albamu hiyo Vanessa na Diamond wameimba kwenye Beat ya S2Kizzy na Laizer walioshirikiana kuikamilisha ‘Far Away’ moja kati ya nyimbo za Diamond ambazo hazikupata atention kubwa.
Katikati ya mwaka 2018, Vanessa na AfricaBoyJux waliungana na wanamuziki wengine kwenye tour yao ya ‘InLoveAndMoney iliyotembea kwenye miji mikubwa ya Tanzania na kupokea positive feedback.

 

Vee Money ni mwanamuziki pekee mwenye Mobile App na website zinazotoa Exclusive zake,Followers milioni 5 kwenye ukurasa wake wa Instagram, mashabiki 380k kwenye twitter yake na subcribers zaidi ya 165,000 kwenye YouTube channel yake yenye views zaidi ya milioni 28 hii inathibitisha na ukubwa wa Vanessa na urefu wa safari yake kwenye muziki. Bendera ya Tanzania inapeperushwa vyema kwenye soko la muziki wa kimataifa popote anopoonekana Vanessa Mdee. Jina la Vanessa Mdee ni miongoni mwa majina yanayochangia mabadiliko mengi na makubwa kwenye jamii ya Tanzania, kupitia muziki wake kuna sehemu ya vijana wenzake wanaonufaika kwa kupata ajira na nafasi ya kufanya kazi na mwanamuziki huyo.

Kwenye intavyuu na Bongo255 ya Global Radio, Vanessa alisema Expensive EP itaachiwa mwaka huu na wakati mashabiki wanaisubiria kwa hamu bado wanaweza kuendelea kusikiliza wimbo wa kwanza kutokea kwenye project hiyo unaotamba kwa jina la Moyo.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey