Mjengo Uliogharimu Mamilioni Ya Travis Scott Na Kylie Jenner
Kumekuwa na tetesi zinazowahusu wanandoa Kylie Jenner na Travis Scott kuachana na kila mmoja kufanya mambo yake. katika hali isiyotegemewa, zimepatikana picha za mjengo wa wawili hao uliopo Beverly Hills, California sehemu ambayo ni mtaa maarufu wanaoishi mastaa wengi wa Hollywood.
picha hizi zimekuja siku za hivi karibuni baada ya kuanza kusambaa tetesi za wawili hao kumwagana, Kylie Jenner alikanusha uvumi huo kwa kusema mapenzi yake na Travis Scott yameongezeka maradufu tangu walipofanikiwa kupata mtoto wao wa kike Stormi Webster.
Imeripotiwa mjengo huu unaogharimu bilioni 30 za Tanzania, unamilikiwa na wote wawili kila mmoja akiwa na asilimia zake hamsini.
5,647 total views, 3 views today
Toa Maoni Yako Hapa