Sambaza

Unyanyasaji Wa Kijinsia Unavyomuumiza Cardi B

Kwa takribani miaka 13 imekuwepo kampeni ya #MeToo inayopinga unyanyasaji wa kijinsia, kampeni hiyo ambayo inapewa nguvu na mastaa wengi wa muziki, imemfikia Cardi B ambaye ameongea ya moyoni kuhusu unyanyanyasaji wa kijinsia unavyowaumiza wasichana wengi.


Kwenye maelezo yake staa huyo wa ‘Press’ amesimulia alivyofanyiwa wakati wa upigaji picha na jarida moja ambalo hakulitaja.
Sitashau nilipokwenda kupiga picha na hili jarida moja ambapo mpiga picha alikuwa anajribu kujiweka karibu na mimi’ Cardi B amesema mpiga picha huyo alimuonyesha tabia za ajabu ikiwa ni pamoja na kumtolea sehemu zake za siri kitu kilichomfanya Cardi achukie na kuondoka kwenye zoezi hilo, hata alipomwambia mmiliki wa jarida hilo hakuna msaada aliouapata.

“Nikiona kampeni ya #MeToo nafarijika kwani, Tabia kama hizi zinawaumiza wasichana wengi ambao wanapambania ndoto zao”. amesema Cardi B.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey