Sambaza

Albamu Ya Kanye ‘Jesus Is King’ Imeghairishwa Tena

Baada ya kusemekana kuna ujio wa albamu yake mpya, Kanye West ameripotiwa kuwa hatoiachia tena albamu hiyo siku ya Ijumaa (Septemba 27) kama ilivyotangazwa mapema. Chanzo cha karibu na Kanye kimewaambia wanahabari kama albamu hiyo haitaachiwa wiki hii.

Ingawa hakuna aliyethibitisha tetesi hizo, Kim Kardashian ambaye ni mke wa Kanye ame-retweet kitu kinachoonyesha kuwa taarifa hizo sio uvumi bali zina ukweli ndani yake, Kwenye tweet hiyo ambayo Kim Kardashian ameshare, maandishi yanasomeka ‘Siku 2 zaidi za Jesus is King’

 

Sio mara ya kwanza kusikia taarifa kama hizi kutokea kwa Kanye, Albamu hiyo ambayo ilitambulika kama ‘Yandhi’  ilitangazwa ingeachiwa Septemba 27,2018 lakini haikuwa hivyo mpaka iliposegezwa mbele mwaka mmoja lakini mambo yanaonekana hayapo tayari kwa albamu hiyo kuachiwa.

Endelea kufuatilia Global Radio, tukipata chochote unachotakiwa kujua kuhusu albamu hiyo, tutahakiksha umekipata kwa wakati.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey