Sambaza

Mzee Chillo: Bongo Muvi Kuna Wavamizi, Wapenda Kiki!..

Mzee Chilo Kwenye Picha Ya Pamoja Na Abdallah Mrisho Ambaye Ni General Manager Wa Global Publishers,

MUIGIZAJI mkongwe katika tasnia ya Bongo Muvi, Mzee Chillo, leo Septemba 26, 2019 amefika katika mjengo wa Global Group, Sinza-Mori jijini Dar es Salaam kufanya mahojiano na Global TV Online na +255 Global Radio. –
Akifanya mahojiano na kipindi cha Mid Morning Fresh cha +255 Global Radio, Chillo amesema sio watu wote ambao wanatoa filamu wana utaalamu wengine wamevamia huku akisema kuwa anajivunia kufahamika tokea ameanza muvi mtaani mpaka Ikulu na amepata nafasi ya kusafiri nje ya nchi na kujuana na watu mbalimbali. –

Pia ameponda tabia ya wasanii kuendekeza kiki kabla ya kutoa kazi huku akisema wanatakiwa kutoa kazi iliyo bora ambayo itapendwa na watu.
Aidha, amewataka baadhi ya madairekta nchini kuacha tabia ya kuwapa wasichana nafasi za kuigiza kwa kigezo cha urembo wao jambo ambalo linadhorotesha tasnia ya uigizaji.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey