Sambaza

Jibu La Aika Kwa Shabiki Anayetaka Kum-Kiss Nahreel Stejini

Moja kati ya matukio ya kiburudani yaliyofanyika Tanzania wiki hii, ni JamaFest ambapo mastaa wengi wa Bongofleva walipata nafasi ya kuburudisha kwenye tamasha hilo lilochukua nafasi kwenye uwanja wa Uhuru Dar Es Salaam.

Kundi la Navykenzo ni miongoni mwa wanamuziki waliotoa burudani ya nguvu usiku wa tukio hilo. Aika kwenye ukurasa wake wa instagram ameposti kipande cha video ya show yake na Nahrel wakiperfom wimbo wao wa ‘Game’. Video inamuonyesha shabiki wa kiume anaepanda jukwaani na  kucheza na Aika huku Nahreel akiendelea kuimba na mashabiki wengine.

View this post on Instagram

Kazini kuna mengi? ?? ??? @2kgrapher #JAMAFEST

A post shared by Aika Marealle (@aikanavykenzo) on

Mmoja kati ya followers wa Aika alitumia uwanja wa Comment kumuuliza Aika kama anaweza kukubali shabiki wa kike kumkumbatia na kumpiga mabusu Baba watoto wake Nahreel. “Hvi Aika kwnye show kma hvyo jmn nikipanda nikamuhug Nahreel na kumkis mabusu kma yte hutonisukuma jukwaan kwl???” , aliuliza shabiki huyo na jibu la Aika lilikuwa hivi “???? haina shida ilimradi kiingilio umelipia???”

Vanessa Mdee ambaye alishirikishwa kwenye wimbo wa Game, ni miongoni mwa waliofurahishwa na jibu hilo kwani hakutaka posti hiyo impite bila kutia neno lolote, kwenye komenti hiyo ambayo imepata replies nyingi ndani ya muda mfupi, Vanessa ameandika “dead ?”.

Wewe unaweza kuruhusu mtu usiyemfahamu amkumbatie mpenzi wako na kumkiss mbele za watu kwa sababu ni shabiki anaekubali kitu kinachofanywa na mpenzi wako?

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey