Pasha: Harmonize Tunashirikiana Sana
Muda mrefu umepita tangu mwanamuziki Pasha amekuwa kimya kwenye muziki. Kwenye kipindi cha Bongo255 kinachoruka +255 Gloal Radio, Pasha amefungukia ishu ya ukimya huo kwa kudai sasa hivi amewekeza zaidi kwenye biashara kuliko muziki.
Pasha alisema ameamua kufanya biashara ya kuingiza magari kutoka nje ya nchi, ufugaji na maduka ya nguo yaliyopo Dar Es Salaam na Mtwara ambako ni asili yake.
Licha ya kuwa kimya kwenye muziki, Pasha amesema zipo projekti zinafanyika huku mojawapo ikiwemo ile ya kushirikiana na Harmonize.
Kuhusu kufanya kazi na Harmonize, Pasha alisema kuwa wasanii wa kusini mwa Tanzania wana ushirikiano na wameamua kuja na kitu ambacho kitawainua wasanii wachanga wanaowakilisha mikoa ya kusini.
Toa Maoni Yako Hapa