Sambaza

Shilole Na Somo La Ndoa Kwa Alikiba

WAKATI msanii Ally Saleh Kiba ‘AliKiba’ ndoa yake ikiwa inapumulia mashine kutokana na migogoro, mrembo kutoka Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shishi’ amempa somo la ndoa msanii huyo kwa kumwambia ndoa inaongozwa na upendo.  Shishi alisema, kutokana na upendo wa dhati walionao yeye na mumewe Uchebe pamoja na hofu ya Mungu waliyonayo ndiyo silaha kubwa ya wao kudumu hivyo kama Kiba na mkewe Amina Khalef hawana hivyo vitu wanapaswa kuvitafuta kwanza.

“Hii ndiyo silaha yangu mimi na mume wangu, hakuna uchawi wala ndumba. Tuna muda mrefu sasa na ndoa yetu ipo imara na hakuna mtu wa kututenganisha,” alisema Shishi au Shilole anayetamba na Wimbo wa Nikagongee Remix aliofanya na Buddest 47.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey