Sambaza

Muigizaji Terrence Howard Amepata Nyota Yake Hollywood Walk Of Fame

Septemba 24,2019 ilikuwa siku kubwa kwa Terrence Howard maarufu kama Lucious Lyon ambaye ni staa wa  tamthilia ya Empire, Muigizaji huyo amepewa heshima ya jina lake kuandikwa kwenye nyota za ‘Hollywood Walk Of Fame’

Kwa mujibu wa DailyMail, nyota yake imepangana na staa mwenzake Taraj P. Henson ambaye kwenye Empire wamecheza kama mke na mume kwenye familia ya wanamuziki. Hii inakuwa nyota ya 2,674 kuwekwa kwenye mtaa huo.

Heshima hii imekuja siku chache baada ya muigizaji huyo kuthibitisha kuwa atastaafu kuigiza mara tu show yake na Fox itakapoisha.

Nyota za ‘Hollywood Walk Of Fame’ hutolewa kwa watu maarufu waliofanya vitu vya kugusa maisha ya wengine, Majina yao huandikwa kwenye mawe yenye umbo la nyota kama heshima kwa mchango wao kwenye jamii.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey