Lil Ommy: Watangazaji Bongo Tuache Ushamba
MFALME wa mahojiano Bongo (King Of Interviews), Omary Tambwe maarufu kama Lil Ommy, THE MVP – amewataka watangazaji nchini kuacha ushamba na kuwasapoti watangazaji wenzao ambao wanafanya kazi ya muziki (watangazaji wanamuziki).
Akipiga stori na kipindi cha Bongo 255 kinachoruka kupitia +255 Global Radio, Ommy ambaye ametajwa kuwania tuzo kubwa za Star QT Awards 2019, kwenye kipengele cha MTANGAZAJI BORA BARANI AFRIKA MWAKA 2019 nchini Afrika Kusini, amesema watangazaji wanapaswa kushirikiana ili kuupeleka muziki wa Bongo mbele.
“Watangazaji wa Bongo tuache ushamba, tuunge mkono harakati za watangazaji wanaofanya muziki. Nimeunga mkono wengi. Kuwasilisha vitu kipekee na tofauti nadhani ndo’ sababu ya kuwa nominated kuwania tuzo za nje.
“Watu wananifuatilia kupitia social media pengine ndo sababu ya kupata nomination nyingi za tuzo nje ya nchi. Kuna watu walinisanua niombe nomination, lakini ilitokea natural tu. Nguvu ya mashabiki imefanya nionekane kwenye list ya watangazaji 10 Afrika.
“Sina uhakika kama kifo cha Ruge Mutahaba kimeifanya value ya muziki wetu ipungue….. Diamond Platnumz amechangia kuleta adabu kwa wasanii, kulipwa vizuri, directors wanalipwa vizuri, vijana wengi kama, Ray Vanny, Mbosso, Lavalava na wengine wengi wamepata maisha kupitia yeye.
“Wizkid alikuwa na management tatu, akawa anatengeneza hela kwa nafasi yake huku anaelewana na watu waliomsaidia, kama Harmonize na Diamond wanaweza kumaliza tofauti zao basi game itakuwa na amani sana.
“Binafsi najiona kama CEO flani hivi ambaye nimetoa mashavu kwa madogo wengi tu. Malengo yangu nilikuwa ni kwenda nje ya Afrika Mashariki, Mungu amebariki vingi sana, natamani kuwa na media house yangu ili nisaidie watu wengine,” amesema Lil Ommy,” anasema Lil Ommy.
Lil Ommy anayeendesha kipindi cha The Playlist kinachoruka Times Fm 100.5 Dar es Salaam, Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 10 hadi saa 12 jioni na pia kupitia chaneli yake ya YouTube, LilOmmyTV, ameseema tuzo hizo zitarajiwa kutolewa Oktoba 26 mwaka huu katika ukumbi wa The Edenvale City jijini Johannesburg, Afrika Kusini.
“Naomba watu wote mnipigie kura kupitia tovuti yao ya www.starqt.com/awards, pia ingia kwenye instagram yangu kuna maelezo namna ya kunipigia kura kwenye tuzo nyingine nilizochaguliwa kuwania,” anasema Lil Ommy.
5,146 total views, 3 views today