Sambaza

Ukweli Kuhusu Pua Ya Michael Jackson

Moja kati ya stori ambazo zinamuongelea kwa ukubwa Michael Jaackson ambaye alikuwa mfalme wa Pop, ni stori ya kuikataa asili yake ya watu weusi na kuamua kuishi mtindo wa maisha ya watu weupe (wazungu). Kumbukumbu huonyesha kama mwanamuziki huyo alikuwa akikumbana na changamoto ya pua yake kudondoka, Hii ilikuwa inasababishwa na upasuaji wa pua ambayo ilichongwa ili ifanane na pua ya kizungu.

 

Kwa mujibu wa Matt Fiddes ambaye alikuwa ni Bodyguard wake, Michael Jackson alijua kama kuna muda maisha yake yatakuwa hayana nguvu kama aliyonayo, alitaka kufanya kitu ambacho macho yote yangekuwa kwake kwa muda mrefu.

Matt amesema Michael alikuwa ni mtu aliyeishi maisha ya kawaida nyumbani kwake lakini alijua jinsi ya kucheza na akili za wanahabari kwa sababu alitaka kukaa kwenye vichwa vya habari kila siku. Inadaiwa kuwa Michael hakubadilisha pua yake bali alikuwa anavaa mpira kwenye pua  ambapo sometimes ulikuwa unaanguka na wanahabari wakajuaa ni pua yake.

Mj alitaka maisha yake yageuke kuwa historia kubwa duniani na hii ndio sababu alikuwa anafanya vitu vingi vinavyohitaji muda wa waandishi wa habari ambao pia walikuwa wanazitafuta sana stori zake.

 

 5,622 total views,  3 views today

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey