Mwaka Mmoja Wa Ndoa Na Hailey, Justin Bieber Ameonyesha Walipoanzia
Baada ya kuonekana pamoja mara nyingi na kuhisiwa kuwa kwenye mahusiano, September 13, 2018 ndiyo siku inayotambulika rasmi kama Justin Bieber aliingia kwenye maisha ya ndoa na mpenzi wake Hailey, ndoa ya Justin na Hailey ni miongoni mwa ndoa za mastaa zinazofuatiliwa karibu kwenye kila kitu wanchokifanya licha ya wao kujitahdi kuishi kwa usiri.
Wakati wanasherehekea mwaka mmoja wa ndoa yao, Supastaa Justin Bieber ameturudisha nyuma mpaka siku za mwanzo mapenzi yao yalipoanzia, wawili hawa wanaonekana waliyaanza mapenzi yao siku nyingi wakiwa na umri mdogo kama unavyoweza kuwaona kwenye picha hii ambayo Bieber ameposti kwenye ukurasa wake wa Instagram akiambatanisha na Caption “My wife and I 🙂 where it all began”
3,238 total views, 3 views today