Sambaza

Kim Kardashian Ametangaza Tarehe Ya Kuachiwa ‘Jesus Is King’ Ya Kanye West

Albamu mpya ya Kanye West Jesus Is King ilikuwa imepangwa kuachiwa rasmi jana (Septemba 27), hata hivyo albamu hiyo ilisogezwa mbele  kwa sababu ambazo hazikujulikana mara moja. Kim Kardashian ambaye ni mke wake ameitangaza jumapili ya Septemba 29 kama siku ambayo albamu hiyo itaingia sokoni.

Kupitia Instagram stori, Kim ameandika kama Kanye anafanya listening party Chicago leo Jumamosi halafu New York kesho Jumapili, kinachosubiriwa ni mixing chache zilizobaki kuikamilisha albamu hiyo yenye nyimbo za dini.

Ujio wa albamu hii ulitangazwa rasmi mwezi August, ambapo mke wa Kanye, Kim Kardashian West ali-post picha yenye orodha ya nyimbo kumi na mbili zilizoambatana na tarehe 27 Septemba. Jana Septemba 28, Kim Kardashian amepost tracklist mpya yenye nyimbo kumi na moja ukiwemo New Body ambao Kanye ameripotiwa kuufanyia kazi kwa muda mrefu.

Mwaka mmoja kabla ya kutangaza ujio wa ‘Jesus Is King’, Kanye alitangaza angeachia ‘Yandhi’, Albamu ambayo ilighairishwa kwa kile ambacho Kanye alisema atatangaza tarehe ya kuiachia atakapokuwa ameikamilisha.

 1,983 total views,  3 views today

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey