Lil Nas X Atangaza Kujipumzisha Kufanya Muziki
Baada ya kuwa stori kubwa kunako anga ya muziki miezi saba iliyopita, Lil Nas X anajipanga kukaa mbali na muziki kwa muda . Ijumaa (Sep 27), Mkali huyo wa wimbo ‘Old Town Road’ ameandika kwenye ukurasa wake wa twitter taarifa hiyo ambayo imezua gumzo kwa mashabiki wake ambao wanaongezeka kila siku.
it’s been a wild last 7 months and im ready to take a little time off. sorry to everyone attending twitchcon or the sandbox music festival, i will not be there. i love u guys and will make it up to you some way. ???
— nope (@LilNasX) September 27, 2019
Lil Nas X mwenye umri wa miaka 20, aliingia kwenye orodha ya wanamuziki waliosikilizwa zaidi mwaka 2019, Hii ni baada ya kuachia wimbo wake ‘Old Town Road’ ambao ni mchanganyiko wa muziki wa Trap na Counrty. Old Town Road imekaa kwenye chati ya muziki ya Billboard Hot 100 kwa wiki 19 mfululizo ikiwa nafasi ya kwanza, Rekodi inayomtaja Lil Nas X kama mwanamuziki wa kwanza wa Hip Hop kumiliki chati muda mrefu.
2,401 total views, 3 views today