Sambaza

Msiba Umeikumba Familia Ya Snoop Dogg

Alhamisi (Septemba 26). mtoto wa Snoop Dogg anayeitwa Corde Broadus, alitumia ukurasa wake wa Instagram kuwataarifu followers wake kuhusu kifo cha mtoto wake aliyeishi siku kumi tu tangu kuzaliwa kwake.

“Kai Love 9/15/19 – 9/25/19 //67/ Mwanangu Kai alituleta upendo mwingi na adabu katika ulimwengu huu, nguvu zake zitaishi na siku hizi 10 za upendo daima zitakuwa maalum kwetu. Wote tuthamini maisha na wale tunaowapenda tukiwa hai. Asante ??.”

Corde hakuiweka wazi sababu ya kifo cha mtoto wake ambaye ni mjukuu wa Snoop Dogg, mke wa Snoop ametumia ukurasa wake wa Instagram kuonyesha ishara ya maombolezo huku Uncle Snoop akiamua kukaa kimya.

 

Mtoto Kai Love alikuwa ni mjukuu wa tano kwa Snoop Dogg ambaye kwa mara ya kwanza alipata mjukuu mwaka 2015, ambapo Corde na mpenzi wake wa zamani walipompata mtoto wa kiume aliyeitwa Zion. Corde ana mtoto mwingine anayeitwa Elleven aliyezaa na Soraya mama wa mtoto Kai aliyefariki.

 4,788 total views,  3 views today

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey