Sambaza

Video Za Kolabo Tano Zinazosumbua Tanzania

Mwanamuziki Innoss’B wa Congo aliungana na mtanzania Diamond Platnumz kuikamilisha Remix ya wimbo ‘YOPE’ ambao umekuwa miongoni mwa nyimbo maarfu za mwaka 2019. Video ya wimbo huu iliachiwa Septemba 7 kupitia YouTube Channel ya Diamond Platnumz, na mpaka sasa zikiwa zimekatika wiki tatu tangu  wimbo huo uwepo, tayari video hiyo imetazamwa zaidi ya mara milioni 10 huku ikiwa nafasi ya kwanza kwenye Video za muziki zinazoangaliwa mara nyingi zaidi wiki hii.

Video hiyo inafuatiwa na video nyingine ambayo ni remix ya ‘Nikagongee’ wimbo wa Baddest 47 kwa ushirikiano na Shilole ambaye ameingia kwenye headlines siku za hivi karibuni baada ya Rostam kumtaja kwenye wimbo wao mpya.

Huo ni ujio mwingine wa Shilole baada ya ukimya wa takribani miezi 7 tangu alipoachia “Ukinitekenya” kwa kushirikiana na Aslay. Video ya Nikagongee Remix inafuatiwa na kolabo ya msafi  Mbosso na mnaijeria Reekado Banks, Shilingi ni wimbo ambao unaosogea taratibu halafu kwa muda mrefu. Ikiwa na zaidi ya wiki moja YouTube, Video ya shilingi imetazamwa zaidi ya mara 998k.

Mbosso kwenye nafasi yake anafuatiwa na Video ya ‘Pepeta’, wimbo wa Nora Fatehi ambaye ni raia wa Canada aliyeshirikiana na Rayvanny wa WCB Wasafi. Video hiyo imekaa youtube kwa wiki mbili na mpaka sasa ina watazamaji zaidi ya milioni 12.

Aslay kwa kushirikiana na King Kiba, waliachia wimbo ‘Bembea’ Septemba 4,2019 , wimbo huu ni miongoni mwa kolabo ambazo zinapata nafasi ya kusikilizwa na video zake kuangaliwa mara nyingi kwa wakati mfupi. Ikiwa inaelekea kumaliza mwezi mmoja kwenye YouTube Chaneli ya Aslay, Bembea imetazamwa zaidi ya mara milioni 1.9

 3,111 total views,  3 views today

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey