Sambaza

Ommy Dimpoz Amepona,Ni Mara Ya Kwanza Kwenye Steji

Mwaka 2018 ulikuwa ni wenye majaribu na chanagamoto kubwa kwa CEO wa PKP, Omary Faraji Nyembo A.K.A Ommy Dimpoz ambaye alitumia zaidi ya miezi 6 hospitalini alikokuwa akipigania afya yake. Kwa mujibu wa Ommy Dimpoz, hicho ndicho kilikuwa kipindi kigumu zaidi katika maisha yake, hivyo hakuona ajabu kumshukuru MUNGU kwa kumuimbia wimbo wa sifa baada ya afya yake kuimarika.

Ni Wewe ulikuwa wimbo wa kwanza wa Ommy Dimpoz tangu atoke hospitali, kwenye wimbo huu Ommy Dimpoz amezisimulia nyakati alizopitia alipokuwa anaumwa. Ni wimbo wenye hisia kali ambao unaweza kuwafariji wenye huzuni na wanaokaribia kukata tamaa.

Kwenye wimbo huo Ommy Dimpoz ameshirikiana na mfalme wa masauti (King Of The The Best Melodies) Christian Bella ambaye anatajwa kuhusika kwa asilimia nyingi kwenye ukamilishwaji wa wimbo huu.

Baada ya Ni Wewe, Ommy Dimpoz ameachia nyimbo nyingine zilizofanikiwa kufanya vizuri zikiwemo Rockstar, You Are The Best, na sasa anatamba na aina mpya ya muziki kwenye mdundo wa Reggaetone na wimbo wake unaoitwa Show Me, Katika kiindi chote alichoanza kuumwa mpaka kuanza kuachia rekodi alizonazo, Ommy Dimpoz hakuwahi kufanya show mbele ya mashabiki zake. Kwa mara ya kwanza Jumamosi (Septemba 28), wakazi wa mwanza walipata bahati ya kuona live show yake kwenye steji ya Tigo Fiesta #SaiziYako na hii hapa ni video ambayo Omary anaonyesha kama yupo vizuri zaidi ya alivyowahi kuwa.

 5,102 total views,  3 views today

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey